Muhimu na hivi sasa… nakala ya khutuma ya Marjaa Dini mkuu kuhusu hali ya taifa kwa sasa

Maoni katika picha
Nakala ya khutuba ya pili iliyotolewa na mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai Ijumaa ya (5 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (31/01/2020m).

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Mabwana na mabibi nakusomeeni nakala iliyotufikia kutoka ofisi ya Mheshimiwa Sayyid katika mji wa Najafu: Imepita miezi minne tangu raia waanze kuandamana na kudai mabadiliko (islahi) ya kulitoa taifa kwenye makucha ya ufisadi na uzembe uliojaa kwenye taasisi nyingi za serikali, damu nyingi imemwagika kwenye maandamano hayo, maelfu ya wananchi wameshambuliwa na kujeruhiwa, bado waandamanaji wanaendelea kushambuliwa hapa na pale, jambo ambalo linaendelea kuongeza idadi ya waathirika.

Kwa mara nyingine Marjaa Dini mkuu analaani utumiaji wa nguvu dhidi ya watu wanaofanya maandamano ya amani, pamoja na kutekwa baadhi yao, aidha analaani vikali utumiaji wa nguvu katika kutawanya watu wanaokusanyika kwa amani, sambamba na kulaani baadhi ya watu wanaoshambulia vikosi vya ulinzi na usalama na mali za serikali, na kushambuliwa kwa baadhi ya taasisi za elimu na huduma zilizo chini ya serikali, na kila jambo linalohusu uvunjaji wa amani na kuhatarisha maslahi yao, anatanabahisha kua vitendo hivyo haviwezi kuzuia kutekeleza madai ya wananchi, bali ni kinyume chake, vinasababisha kushikamana zaidi na maandamano pamoja na kuongeza idadi ya waandamanaji.

Kuendelea kukosekana utulivu wa kisiasa, kiuchumi na amani hakuna faida kwa taifa wala mustakbali wa raia, lazima tuondoke katika hali hiii kwa kuunda serikali mpya haraka, itakayo kubalika na kuaminika na raia, inayo weza kutuliza mambo na kurudisha haiba ya serikali sambamba na kuandaa uchaguzi huri na wa haki.

Kurudi kwenye masanduku ya kura na kuwapa fursa wananchi ya kuchagua viongozi wanao wataka ndio jambo linalo takiwa kwa sasa, pamoja na mpasuko wa vyama vya kisiasa, na kutofautiana kwa mitazamo yao pamoja na vipao mbele vyao katika hatua ijayo, sambamba na kushindwa kukubaliana katika kutatua mambo yanayodaiwa na wananchi, jambo linalo endelea kuliweka taifa katika hatari na matatizo, dawa ya matatizo yote ni kufanya uchaguzi wa mapema na kuwapa wananchi waamue wanacho taka, bunge lijalo liwe huru na lenye uwezo wa kufanya maamuzi ya lazima na kuunda kanuni zenye maslahi na mustakbali wa taifa, hususan yanayohusu haki na uhuru wa maamuzi ya kisiasa pamoja na umoja wa taifa na raia.

Mwisho: Marjaa Dini analaani vikali njama dhalimu ya hivi karibuni katika ardhi ya Palestina inayo kaliwa kimabavu, anasisitiza kusimama pamoja na raia wa Palestina katika kudai haki ya kurudi katika ardhi yao inayo kaliwa kimabavu na kuunda taifa huru, anatoa wito kwa waarabu na waislamu pamoja na kila mpenda amani duniani ashikamane nao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: