Marjaa Dini mkuu amerudia kukemea utumiaji wa nguvu dhidi ya watu wanaofanya maandamano ya amani pamoja na kutawanya mikusanyiko ya watu kwa kutumia nguvu, sambamba na ushambuliaji na utekaji wa waandamanaji, akasisitiza kua vitendo hivyo haviwezi kuzuwia mikusanyiko ya watu na kutotekeleza madai yao, bali kinyume chake inasababisha watu waungane zaidi na maandamano.
Yamesemwa hayo katika khutuba ya Ijumaa leo (5 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na 31 Januari 2020m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:
(Imepita miezi minne tangu raia waanze kuandamana na kudai mabadiliko (islahi) ya kulitoa taifa kwenye makucha ya ufisadi na uzembe uliojaa kwenye taasisi nyingi za serikali, damu nyingi imemwagika kwenye maandamano hayo, maelfu ya wananchi wameshambuliwa na kujeruhiwa, bado waandamanaji wanaendelea kushambuliwa hapa na pale, jambo ambalo linaendelea kuongeza idadi ya waathirika.
Kwa mara nyingine Marjaa Dini mkuu analaani utumiaji wa nguvu dhidi ya watu wanaofanya maandamano ya amani, pamoja na kutekwa baadhi yao, aidha analaani vikali utumiaji wa nguvu katika kutawanya watu wanaokusanyika kwa amani, sambamba na kulaani watu wanaoshambulia vikosi vya ulinzi na usalama na mali za serikali, na kushambuliwa kwa baadhi ya taasisi za elimu na huduma zilizo chini ya serikali, na kila jambo linalohusu uvunjaji wa amani na kuhatarisha maslahi yao, anatanabahisha kua vitendo hivyo haviwezi kuzuia kutekeleza madai ya wananchi, bali ni kinyume chake, vinasababisha kushikamana zaidi na maandamano pamoja na kuongeza idadi ya waandamanaji).