Marjaa Dini mkuu: Kuharakisha kuundwa serikali mpya ndio njia ya kumaliza matatizo tulionayo

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu kwa mara nyingine tena amerudia kutoa wito wa kuundwa haraka serikali mpya itakayo aminiwa na wananchi, yenye uwezo wa kutuliza hali na kuandaa haraka uchaguzi huru na wa haki.

Ameyasema hayo katika khutuba ya swala ya Ijumaa leo (5 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (31 Januari 2020m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Kuendelea kukosekana utulivu wa kisiasa, kiuchumi na amani hakuna faida kwa taifa wala mustakbali wa raia, lazima tuondoke katika hali hii kwa kuunda serikali mpya haraka, itakayo kubalika na kuaminika na raia, inayo weza kutuliza mambo na kurudisha haiba ya serikali sambamba na kuandaa uchaguzi huru na wa haki).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: