Marjaa Dini mkuu: Kurudi kwenye masanduku ya kura na kuwaacha wananchi wachague viongozi wanao wataka ndio njia sahihi ya kumaliza matatizo tulionayo

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu ameongea kuhusu hali inayo endelea kwa sasa kua, kurudi kwenye masanduku ya kura na kuwaacha wananchi wachague viongozi wanao wataka ndio njia sahihi ya kumaliza matatizo tuliyo nayo, bunge lijalo litokane na matakwa ya raia na liwe tayali kufanya mabadiliko (islahi).

Ameyasema hayo katika khutuba ya swala ya Ijumaa leo (5 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (31 Januari 2020m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai. Lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Kurudi kwenye masanduku ya kura na kuwapa fursa wananchi ya kuchagua viongozi wanao wataka ndio jambo linalo takiwa kwa sasa, pamoja na mpasuko wa vyama vya kisiasa, na kutofautiana kwa mitazamo yao na vipao mbele vyao katika hatua ijayo, sambamba na kushindwa kukubaliana katika kutatua mambo yanayodaiwa na wananchi, jambo linalo endelea kuliweka taifa katika hatari na matatizo, dawa ya matatizo yote ni kufanya uchaguzi wa mapema na kuwapa wananchi waamue wanacho taka, bunge lijalo liwe huru na lenye uwezo wa kufanya maamuzi ya lazima na kuunda kanuni zenye maslahi na mustakbali wa taifa, hususan yanayohusu haki na uhuru wa maamuzi ya kisiasa pamoja na umoja wa taifa na raia).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: