Marjaa Dini mkuu amelaani kinachoitwa (Swafhatul-Qarni) na amesisitiza kuwaunga mkono raia wa Palestina.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amelaani vikali kile alicho kiita mkakati dhalimu uliotangazwa hivi karibuni unaowapa haki mazayuni ya kuendelea kupora ardhi ya wapalestina, amesisitiza kuwaunga mkono raia wa Palestina kua na haki ya kurudi katika taifa lao.

Ameyasema hayo katika khutuba ya Ijumaa leo (5 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (31 Januari 2020m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Marjaa Dini analaani vikali njama dhalimu ya hivi karibuni katika ardhi ya Palestina inayo kaliwa kimabavu, anasisitiza kusimama pamoja na raia wa Palestina katika kudai haki ya kurudi katika ardhi yao inayo kaliwa kimabavu na kuunda taifa huru, anatoa wito kwa waarabu na waislamu pamoja na kila mpenda amani duniani ashikamane nao).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: