Chuo kikuu cha Alkafeel na mkakati wa kupunguza muda wa masomo.

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed katika mkoa wa Najafu chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kupunguza muda wa masomo kwa asilimia %10 katika mwaka huu, ili kupunguza usumbufu kwa wanafunzi na walezi wao hususan katika wakati tulionao, na kua msaada kwao wa kukamilisha safari ya elimu yao.

Uongozi wa chuo umeuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kupunguza huko kunatokana na malengo ya kuanzishwa chuo, na juhudi ya kuhakikisha kinakua moja ya taasisi bora za kielimu chini ya viwango vya ufundishaji na utafiti vya kimataifa, sambamba na kuhudumia jamii sawa na mahitaji ya maendeleo ya kibinaadamu, chini ya misingi ya kitaifa na kiislamu”.

Kutokana na jambo hilo wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu imeshukuru msimamo huo wa kibinaadamu, aidha wazazi wa wanafunzi wamekishukuru chuo kwa kuwa msaada kwao daima na kuhakikisha vijana wao wanaendelea na masomo.

Tambua kua chuo kikuu hicho kina jumla ya wanafunzi (3766) katika vitivo vifuatavyo (udaktari wa meno, famasiyya, sheria, uhandisi, tiba na afya) na kuna vitengo vingine vitatu ambavyo ni: (sheria, habari na utalii wa kidini).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: