Masanduku ya amanaat ni njia nzuri ya kuhifaddhi vitu vya mazuwaru

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kupunguza uzito kwa watu wanaokuja kutembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuwapa uhuru wa kuhifadhi vifaa vyote bila usumbufu, Atabatu Abbasiyya tukufu imeweka masanduku mengi ya kuhifadhia vitu katika maeneo ya haram tukufu.

Masanduku hayo yameondoa usumbufu wa kusimama kwenye mistari muda mrefu kwa ajili ya kuweka au kuchukua vifaa vyao, hali kadhalika yamepunguza kazi kwa watumishi ya kupokea na kutoa vitu vya mazuwaru, sambamba na hilo matumizi yake ni rahisi.

Masanduku ni sehemu ya huduma muhimu wanazo pewa mazuwaru na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuwaondolea usumbufu uliopo kwenye mabanda ya kuweka vitu (amanaat), yamewekwa kwa utaratibu mzuri usioruhusu msongamano wala kutatiza shughuli za upanuzi.

Kila sanduku linaufunguo wenye namba ya sanduku husika na mahala lilipo, zaairu huweka vitu vyake ndani na kuchukua funguo kisha kuufunga mkononi, baada ya kumaliza kufanya ziara hurudi na kuchukua vitu vyake halafu ufungua anauacha sehemu husika, kitengo cha usimamizi wa kihandisi kinaangalia masanduku hayo muda wote, kwa ajili ya kufanyia matengenezo ya haraka sanduku lolote litakalo haribika.

Mradi huu ni msaada mkubwa kwa kitengo cha zamani cha Amanaat, na umewapa nafuu sana mazuwaru, wamezishukuru Ataba tukufu husasan Atabatu Abbasiyya kwa kuweka huduma hii katika mji ambao ni kibla ya wapenzi na tulizo la mazuwaru Karbala takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: