Kumbukumbu ya kifo cha Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Bado sauti ya kumbukumbu ya kifo cha mtoto wa Mtume bibi Zaharaa (a.s) inaendelea kusikika, Maahadi ya Quráni chini ya Atabatu Abbasiyya kupitia tawi lake la mkoa wa Najafu imeandaa majlisi kubwa ya kuomboleza msiba huo, na kuhudhuriwa na kundi kubwa la waumini.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, halafu ukafuatia mhadhara wa kielimu uliotolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Ashkuri, ameongea mambo muhimu yanayo husu jamii na itikadi, akabainisha kua Zaharaa (a.s) alipata shahada kwa ajili ya kutetea jambo la wazi lililokua limesha semwa na Mtume (s.a.w.w) siku ya Ghadiir.

Majlisi ilihitimishwa kwa tenzi za kuomboleza kutoka kwa Shekh Abdullahi Dujaili, zilizo elezaea msiba wa Zaharaa (a.s) na mitihani aliyopata kiongozi wa waumini (a.s), wakielekeza nyoyo zao kwa kilele wa kujitolea na mlango wa haja Abulfadhil Abbasi (a.s).

Fahamu kua Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo vyake mbalimbali hufanya majlisi katika matukio yote ya Ahlulbait (a.s), pamoja na kumbukumbu ya kifo cha mbora wa wanawake wa duniani (a.s) kwa riwaya zake zote tatu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: