Shindano la kitaifa kwa wanawake la kuhifadhi Quráni tukufu lamalizika

Maoni katika picha
Kufuatia kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu isemayo: (Mwisho wake ni miski, na katika hilo washindane wenye kushindana) baada ya siku tatu za mashindano ya Quráni, Maahadi ya Quráni tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya wamemaliza mashindano ya Quráni ya wanawake awamu ya tatu, yaliyokua na washiriki (63) kutoka mikoa tofauti, walipata nafasi ya kushiriki kwenye mashindano haya baada ya kushinda mashindano ya awali, ambayo hulenga kuandaa wasomaji na mahafidh wa Quráni, na washiriki wa mashindano haya ndio ambao hupewa nafasi za kushiriki mashindano ya kimataifa.

Mahafidhi wamewekwa kwa vikundi, mashindano yamefanywa siku tatu mfululizo, chini ya mazingira mazuri ya kiroho yaliyojaa nuru ya Quráni tukufu, sauti nzuri za usomaji wa Quráni zikisikika, mashindano ya kuhifadhi Quráni yanaanzia juzuu tano hadi Quráni yote.

Washindi wa mashindano haya ni:

Kwanza: Washindi wa kuhifadhi Quráni yote:

Zaharaa Abduljabaar.

Zaharaa Ahmad Majiid.

Suruuq Najaah.

Pili: washindi wa kuhifadhi juzuu ishirini:

Dhuha Hussein Halo.

Shahidi Hussein.

Zaharaa Ali Hashim.

Tatu: washindi wa kuhifadhi juzuu kumi na tano:

Aliya Abduljabaar.

Nagham Rasuli Aufi.

Nuru Ali Rahim.

Nne: washindi wa kuhifadhi juzuu kumi:

Zainabu Muthanna Khalid.

Fatuma Maajid Hamiid.

Qamaru Duriid Muiin.

Tano: washindi wa kuhifadhi juzuu tano:

Zuhura Swadiq Ali.

Baniin Rahmaan Jabari.

Manaar Alawi Jawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: