Tunakulisheni kwa mikono yetu je ni sawa na utukufu wenu?

Maoni katika picha
Tangu kutolewa kwa fatwa tukufu ya jihadi kifaya, mawakibu za kutoa misaada zilizopo chini ya idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya hazija acha kuwasaidia wale walio itikia wito huo, zimekua pamoja nao hadi kwenye uwanja wa vita, zimetoa mashahidi na kuchanganyika damu zao na zile za wapiganaji, wamepita njia ya kifo, wanamchango mkubwa katika ushindi, waligawa asilimia kubwa ya vitu vilivyo kua vinahitajiwa na wapiganaji kwa kuzingatia mazingira na wakati.

Kazi zao hazikuishia katika uwanja wa vita peke yake, bali ziliendelea na bado zinaendelea hadi sasa, kinacho fanywa na maukibu yake ya Najafu ni mfano wa huduma nyingi zitolewazo, mawakibu hizo zinamchango mkubwa ambao ulishuhudiwa na vikosi vyote vya wapiganaji, leo hii ndani ya siku tatu mfululizo pamoja na ukali wa baridi msafara wa vijana wa Muntadhar (a.f) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu/ Idara ya Najafu na Kufa, wanapika na kugawa milo mitatu ya chakula kwa jina la (zawadi ya Ahlulbait –a.s-) kwa wapiganaji wa jeshi la serikali na Hashdi Shaábi Liwaa/44 Answaru Marjaiyya katika mkoa wa Mosul – wilaya ya Hadhar.

Kiongozi wa msafara huo Ustadh Aqiil Mahbuba amesema kua: Idara ya Najafu inaharakati kubwa katika sekta hii, siku za nyuma ilipeleka misaada kwa vikosi vya wapiganaji waliopo kwenye uwanja wa vita, pamoja na kutoa misaada kwa mafakiri na watu wenye mahitaji maalum sambamba na kuzitembelea familia za mashahidi, hatukuzuwiwa na kikwazo chochote kutekeleza wajibu wa kidini, kitaifa na kibinaadamu, furaha yetu ni kufanya hivyo, tunawashukuru waliosaidia na kufadhili msafara huu.

Akasisitiza kua: “Hatujatosheka na kugawa tulicho jaliwa peke yake, bali tumepika chakula na kuwapa kwa mikono yetu, hakika wao wanahaki zaidi kwetu, je tunaweza kufikia utukufu wao?”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: