Chuo kikuu cha Alkafeel chaeleza mkakati wake na miradi ijayo

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya idara ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imejata mkakati wake wa maboresho kama ifuatavyo:

Kwanza: kufungua vyuo na vitengo vipya vya elimu.

Pili: kuajiri walimu wenye uwezo mkubwa.

Tatu: kusimamia ubora wa elimu katika vyuo vikuu vya kitaifa na kimataifa.

Nne: kusaidia katika kuandaa program za tafiti za kielimu na kuzisambaza kwenye majarida ya kitaifa na kimataifa, kwa lengo la kuboresha harakati za vitengo vya Atabatu Abbasiyya na kutatua changamoto za jamii.

Tano: kuratibu harakati za kitamaduni (nadwa, warsha na makongamano ya kitaifa na kimataifa) kwa lengo la kuongeza ujuzi.

Sita: mkakati wa kuanzisha masomo ya juu.

Saba: kuweka uhusiano mwema na vyuo vikuu vya Iraq na vya kimataifa kupitia makubaliano maalum.

Kumbuka kua idadi ya wanafunzi katika vitivo na vitengo vyote wanafika (3766), ambao wapo katika vitivo vifuatavyo (udaktari wa meno, famasia, sheria, uhandisi, tiba na afya) na kuna vitengo vitatu ambavyo ni: (sheria, habari na utalii wa kidini), kuna walimu mahiri waliobobea katika fani mbalimbali pamoja na idara makini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: