Hospitali ya Alkafeel imefanya upasuaji (8815) ndani ya mwaka wa 2019 kwa mafanikio ya asilimia %98.

Maoni katika picha
Mkuu wa hospitali ya Alkafeel Dokta Jaasim Ibrahim amesema kua mwaka jana walifanya upasuaji (8815) na walifanikiwa kwa asilimia %98.

Akasisitiza kua: Asilimia kubwa ya upasuaji huo ulikua ni vigumu kufanyika hapa Iraq miaka ya nyuma, na umefanywa na madaktari wazawa kutoka ndani na nje ya Iraq pamoja na waarabu na wasiokua waarabu.

Akaongeza kua: “Miongoni mwa upasuaji tuliofanya ni upasuaji wa moyo, saratani, mifupa, figo na aina zingine”.

Akasema kua: “Vifaa vya kisasa vilivyopo hospitali na umahiri wa madaktari ndio sababu ya mafanikio, tumeweza kutoa huduma za matibabu kwa wairaq na kuwapunguzia mzigo wa kwenda nje ya taifa kutafuta matibabu”.

Tambua kua idara ya hospitali ilitangaza kua vyumba vyake vya upasuaji ni vya kisasa na vina vifaa bora vinavyo endana na hospitali kubwa za kimataifa kwenye nchi zilizo endelea (I.S.O).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: