Kazi inaendelea mwaka mzima wala haina msimu maalum… imeoteshwa na shamba boy wa Alkafeel.

Maoni katika picha
Kazi za shamba boy wa Alkafeel haziishii Atabatu Abbasiyya peke yake au katika msimu maalum, bali wanafanya kazi mwaka mzima kwa kuotesha miche inayo endana na kila msimu katika mwaka, hivi karibuni wametangaza kuotesha aina mpya za miche ya msimu na isiyokua na msimu, inayo endana na hali ya hewa ya Karbala pamoja na mikoa mingine.

Kiongozi wa shamba boy wa Alkafeel Ustadh Muayyad Hatifu Muhammad amesema kua: “Kazi yetu ya kuotesha miche huendelea mwaka mzima chini ya utaratibu maalum, hatuna msimu maalum, kutokana na uchache wa miche ambayo huoteshwa wakati wa masika, tumeamua kuingiza aina mpya ya miti mikubwa na midogo, pamoja na miti ya msimu na ya kivuli, zikiwemo aina ambazo zimeingia Iraq kwa mara ya kwanza”.

Hatifu amefafanua kua: “Kuna mwitiko mkubwa wa miche yetu kwa sababu nyingi, miongoni mwa sababu hizo ni:

  • - Ubora wa miche.
  • - Uhusiano mwema.
  • - Kuheshimu muda.
  • - Tuna mawakala wanaosaidia kusambaza baadhi ya miche yetu.
  • - Sisi ni watu pekee ambao tunaotesha baadhi ya miche kwa kiwango kikubwa na muda mfupi”.

Mwishoni mwa maongezi yake akasema kua shamba boy wa Alkafeel wako tayali kuotesha miti ya mauwa kulingana na mahitaji ya taifa, inayo endana na mazingira ya hali ya hewa tena kwa bei nafuu, unaweza kwenda kuangalia aina ya miti ya mauwa unayo hitaji katika vituo vyetu vya mauzo mubashara, au wasiliana na uongozi wa shamba boy katika Ataba tukufu kupitia sim namba (07718003738) au tembelea eneo letu katika mkoa wa Karbala/ barabara ya Husseiniyya/ karibu na bango jeupe, au vituo vya mauzo mubashara katika barabara ya Jamhuriyya – karibu la duka la Rafidina, katika mtaa ya Hussein (a.s) – kituo cha Afaaf cha kibiashara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: