Utangulizi wa msaada wake kwao: kamati ya ustawi wa jamii yawasili mashariki ya Biji.

Maoni katika picha
Katika muendelezo wa harakati zake za awali tangu ilipo tolewa fatwa ya jihadi kifaya wa kuwasaidia wale walio itikia fatwa hiyo, kamati ya ustawi wa jamii chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya imewasili katika mkoa wa Swalahu Dini (mashariki ya wilaya ya Biji), kwa wapiganaji wa Liwaa/35 Hashdi Shaábi wanao linda amani eneo hilo, kuwapatia khairaati (misaada) kutoka kwa mkarimu Abulfadhil Abbasi (a.s).

Shekh Haidari Aaridhwi kiongozi wa kamati ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya alikuwepo katika msafara huo na ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kutokana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu ya kuwasaidia wapiganaji waliopo sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kikosi cha Swalahu Dini”.

Akasema: “Tumewakuta wapiganaji wakiwa na hamasa kubwa pamoja na ugumu wa mazingira ya hali ya hewa na uhaba wa vifaa, wamesimama imara kuhakikisha magaidi hawarudi tena katika ardhi ya Iraq, baada ya kuikomboa kutokana na utukufu wa damu za wapenzi wao, leo wamesimama imara dhidi ya kila anayetaka kuharibu amani na utulivu wa taifa hili”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya hutuma misafara ya kutoa misaada ya chakula na vitu vingine kwa vikosi vyote vya wapiganaji, aidha imeunda kamati maalumu kwa ajili ya kusaidia familia za mashahidi na kufuatilia hali za majeruhi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: