Hatua ya mwisho katika mradi wa upanuzi wa Maqam ya Imamu Mahadi (a.f).

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaighi amesema kua wameingia hatua ya mwisho katika mradi wa upanuzi wa Maqam ya Imamu Mahadi (a.f), hadi sasa kazi imesha kamilika kwa asilimia tisini (%90), inatarajiwa kukamilika mwezi wa Shabani mwaka huu katika siku za kukumbuka kuzaliwa kwa muokozi wa walimwengu mwenye Maqam hiyo tukufu.

Akaongeza kua: “Hatua ya mwisho inahusisha kuweka Kashi Karbalai sehemu ya ndani na kuweka marumamru na vioo vilivyo katwa kitaalam na kuwekwa nakshi na mapambo sambamba na maandishi”. Akasema: “Hali kadhalika tumefunga mfumo wa umeme, utowaji wa tahadhari, zima moto, mawasiliano, ulinzi na mingineyo, baada ya kumaliza kufunga nyaya za umeme na kujenga mnara wa saa uliopo juu ya paa sehemu ya katikati upande wa mbele”.

Fahamu kua upanuzi umehusisha eneo la wanawake lenye ukubwa wa mita za mraba (490) takriban, sehemu ya pili imehusisha ukumbi wa wanaume wenye ukubwa wa mita za mraba (310) na sehemu ya watumishi wa Maqam yenye ukubwa wa mita za mraba (150) sehemu iliyo baki ni ya vyoo, vilevile tumefanya upanuzi katika lango kuu kwa ndani na nje, tumeweka pambo lenye upana wa zaidi ya mita nne na pembezoni mwake kuna nguzo.

Kumbuka kua Maqam ya Imamu Mahadi (a.f) ipo upande wa kushoto wa mto wa Husseiniyya wa sasa unapo ingia Karbala kwa kutumia barabara inayopita katika Maqam ya Imamu Jafari Swadiq (a.s) nayo ni mazaru mashuhuri, Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua jukumu la kufanya matengenezo makubwa, kuanzia kwenye kubba hadi kumbi za haram na maeneo mengine, kwa kua sehemu ilipo Maqam hauwezi kufanya upanuzi katika pande zake tatu, ililazimika kufanya upanuzi upande wa mto wa Husseiniyya ambao ni upande wa magharibi, kwa kujenga nguzo na kuweka juu yake mfano wa daraja bila kuzuwia maji wala kubadili njia yake, jumla la eneo lililo ongezwa linakadiriwa kua mita za mraba (1200) linaungana na Maqam kwa kutumia milango maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: