(Kichuguu cha Zainabiyya kiadabu na kimaumbile) semina ya kuandaa mubalighaat:

Maoni katika picha
Maahadi ya turathi za mitume (a.s) ya masomo ya hauza kwa mtandao na chuo kikuu cha Ummul Banina (a.s) chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, imeazimia kufanya semina ya tatu ya kuandaa mubalighaat chini ya anuani isemayo: (Kichuguu cha Zainab kiadabu na kimaumbile).

Semina hii ni sehemu ya kuendeleza mafanikio yaliyo patikana katika semina za siku za nyuma, kutokana na umuhimu wa tablighi kwa wanawake hususan wakati wa msimu wa maombolezo, ili kuwatoa pembezoni kupitia mitazamo na fikra za kisasa kuhusu maombolezo ya kudumu ya Husseiniyya chini ya utaratibu unao fahamika na ulio karibu na uhalisia.

Program ya masomo yafuatayo imeandaliwa kwa muhtasari:

  • 1- Masomo ya Fiqhi.
  • 2- Masomo ya Akhlaq.
  • 3- Masomo ya Aqida.
  • 4- Masomo ya Sira za Maimamu watakasifu (a.s).
  • 5- Mihadhara kuhusu mimbari ya Hussein.

Wakina dada wanaopenda kushiriki wawasiliane na uongozi wa kitengo cha wanawake cha Maahadi na chuo kupitia telegram kwa namba: (07602421256).

Washindi watatu wa mwanzo kwenye semina hiyo watapewa zawadi kama ifuatavyo:

  • 1- Mshindi wa kwanza: laki mbili na elfu hamsini (250,000) dinari za Iraq.
  • 2- Mshindi wa pili: laki moja na elfu hamsini (150,000) dinari za Iraq.
  • 3- Mshindi wa tatu: laki moja (100,000) dinari za Iraq.

Kwa maelezo zaidi na maswali fungua link ifuatayo: https://t.me/turathmanage
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: