Ni bure.. mradi wa kufuta ujinga katika Atabatu Abbasiyya umefungua milango ya usajili na umetoa wito kwa kila anayetaka kushiriki aje kujiandikisha

Maoni katika picha
Katika kuendeleza mafanikio yaliyo patikana kwenye semina za awali, mradi wa kufuta ujinga ambao ni moja ya miradi inayo fadhiliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, umefungua mlango wa usajili (elimu ya msingi) kwa ajili ya kupunguza idadi ya wasiojua kusoma na kuandika, wanaopenda kushiriki wafanye haraka kuandikisha majina yao na wanufaike na fursa hii.

Uongozi umeandaa walimu wawili mahiri na wenye uzowefu mkubwa, wamesha shiriki semina nyingi kuhusu njia bora za ufundishaji.

Masharti ya kujiandikisha ni:

  • 1- Usiwe chini ya umri wa miaka (15).
  • 2- Uwe haujui kuandika na kusoma.

Idara imesema kua watu wanaweza kwenda kujisajili katika ofisi zake zilizopo kwenye jengo la Imamu Askariy (a.s) mkabala na hospitali ya mlango wa Bagdad (Baabu Bagdad), kwa maelezo zaidi piga simu namba: (07602323721/ 07723771314).

Fahamu kua atakaehitimu masomo hayo atapewa cheti cha kujua kusoma na kuandika kinacho tambuliwa na wizara ya malezi na elimu ya Iraq.

Tambua kua mradi huu ulianza kutekelezwa baada ya kupewa kibali na wizara ya malezi na elimu pamoja na uongozi wa malezi na elimu wa mkoa wa Karbala, chini ya walimu waliopewa mbinu maalumu za ufundishaji kupitia semina mbalimbali, sambamba na kuandaa sehemu maalum za kusomea, tumechagua Husseiniyya na majengo yaliyopo katika mitaa ya mji wa Karbala kwa ajili ya kusomeshea, cheti cha kufuta ujinga kinalingana na mtu aliye maliza darasa la nne katika shule ya msingi, mitihani wanayo fanya watu wanaomaliza elimu hiyo huandaliwa na wizara ya malezi na elimu, iko sawa na ile ya kumaliza elimu ya msingi inayojulikana kitaifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: