Viatu vinahifadhiwa katika utaratibu mzuri

Maoni katika picha
Watumishi wa idara inayo simamia senemu za kuvulia viatu (kashwaniyya) chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, idara ambayo ainafanya kazi moja kwa moja na mazuwaru usiku na mchana kwa ajili ya kumhudumia kila anaekuja kumtembelea Abulfadhil Abbasi (a.s), miongoni mwa mafanikio makubwa ya idara hiyo ni kuweka utaratibu mzuri kwa mazuwaru wa uwekaji na uchukuaji wa viatu, pamoja na kua na subira ya hali ya juu katika kuwahudumia.

Kila mlango katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kuna sehemu za kuweka viatu (kashwaniyya), kila sehemu ina alama ya herufu maalum na rangi tofauti na mlango mwingine, kwa ajili ya kurahisisha kupaelewa na kupafikia baada ya umaliza kufanya ziara.

Sehemu za kuvulia viatu zinazo zunguka haram tukufu zimefika (43), za wanaume na wanawake.

Kazi ya kupokea na kutoa viatu inafanywa kwa kutumia utambulisho wa namba zenye alama maalum zinazo tofautiana na kila sehemu, watumishi wa idara hiyo wanafanya kazi saa (24) kila siku, wala kazi yao haiishii kwenye viatu peke yake, bali wanawasaidia pia mazuwaru wenye umri mkubwa na wenye ulemavu kuwapeleka ndani ya haram tukufu, na kuwawezesha kufanya ziara kwa kutumia viti vya mataili.

Tambua kua watumishi wa idara ya viatu wana sifa nyingi, hupewa semina mbalimbali za kidini na kiutamaduni ili kuwaandaa waweze kuamiliana vizuri na mazuwaru, pamoja na kufundishwa lugha tofauti ili waweze kuwasiliana na wageni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: