Katika washiriki (8228) kutoka zaidi ya nchi 22: Mpiga picha wa Atabatu Abbasiyya tukufu aibuka mshindi wa kwanza katika shindano la kimataifa.

Maoni katika picha
Mpiga picha wa kituo cha uzalishaji na upigaji picha Alkafeel chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu bwana Saamir Khaliil Ibrahim Husseini amekua mshindi wa kwanza kwenye shindano la kimataifa la upigaji picha, linalo simamiwa na wizara ya utamaduni ya Iran na kufanyika chini ya anuani isemayo kumpenda Hussein (hubu Hussein), washiriki wa shindano hilo walikua (8228) kutoka kwenye nchi zaidi ya (20) ikiwemo Iraq.

Kushiriki kwenye shindano hili na kupata tuzo ni moja ya mfululizo wa tuzo ambazo wamekua wakizipata wapiga picha wa Atabatu Abbasiyya tukufu, sawa yawe mashindano ya kitaifa au kimataifa, kutokana na uzuji na uzowefu mkubwa walionao unawawezesha kupata tuzo hizo, sambamba na msaada wanaopewa na viongozi wa idara zao, chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya ambao umekua ukijitahidi kuwajengea uwezo watumishi wake wote.

Fahamu kua ushindi huu sio wa kwanza, amesha wahi kushiriki na kushinda kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa, hivyo ushindi huu ni sehemu ya muendelezo wa ushindi aliopata siku za nyuma na nimatarajio yetu hautakua wa mwisho.

Kumbuka kua vitengo vya Atabatu Abbasiyya na watumishi wake hushiriki kwenye mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa, wamefanikiwa kushinda na kupata tuzo mbalimbali katika setka tofauti, kutokana na ushirikiano wanaopewa pamoja na uaminifu (ikhlasi) kwenye kazi zao kwa ajili ya kupandisha bendera ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: