Chuo kikuu cha Ummul Banina (a.s) kimeondoa kizuwizi cha umbali katika kufikia kisima cha maarifa.

Maoni katika picha
Kutokana na malengo makuu ya mapinduzi ya Twafu yaliyokua na bado yanaendelea kufundisha ubinadamu, ili kujenga kizazi cha mubalighaati wenye uwezo wa kufanyia kazi malengo ya mapinduzi ya Imamu Hussein (a.s) katika khutuba zao na maelekezo yenye misingi madhubuti ya kielimu, chini ya selebasi (manhaji) iliyo andaliwa na walimu wazowefu katika mji wa Najafu, chuo kikuu cha Ummul Banina (a.s) kimeanzisha masomo ya kuandaa mubalighaat kwa njia ya mtandao (masafa).

Uzinduzi huu umefanywa baada ya kupata mafanikio katika mradi wa Maahadi ya turathi za mitume (a.s) ya masomo ya hauza kwa njia ya mtandao (masafa), mradi huu umepata mwitikio mkubwa kutoka kwa vijana wa sehemu tofauti, kwani kizuwizi kikubwa kati yao na kisima cha elimu mjini Nafafu kilikua ni umbali.

Kizuwizi hicho kimevunjwa kwa kufungua masomo kwa njia ya mtandao (masafa) ya kuandaa mubalighaat, muda wa masomo ni miaka minne, miaka mitatu ya masomo kwa nadhariyya na mwaka mmoja wa masomo kwa vitendo, ambapo watatoa mawaidha na kufanya tablighi ndani na nje ya Iraq.

Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: