Makundi ya waombolezaji yawasili katika ardhi takatifu na mgahawa waona fahari kuwahudumia

Maoni katika picha
Makundi ya waombolezaji yamewasili katika ardhi takatifu ya Karbala, katika kumbukumbu ya kifo cha bibi wa kujitolea Ummul Banina (a.s), na kumpa pole mfiwa mkuu ambae ni mtoto wake mwezi wa familia (a.s) na kipenzi wake bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s).

Kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya kwenye matukio kama haya kimezowea kuongeza huduma kwa utaratibu maalum, huongeza ugawaji wa chakula na vinywaji kwa waombolezaji watukufu, ambao huwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na kulinda taifa la Iraq lisipate matatizo, humuomba Mwenyezi Mungu kwa utukufu wake kama alivyo tuamrisha.

Kitengo cha mgahawa kimefungua sehemu mbili kwa ajili ya kugawa chakula kwenye tukio hili chungu, ili kuweza kufikia idadi kubwa ya mazuwaru, wanaokuja kutoka mikoa tofauti ya taifa letu kipenzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: