Katika kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha bibi mtukufu Ummul Banina (a.s); Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ndani ya haram ya mwanae mwezi wa familia Abulfadhil Abbasi (a.s).
Majlis zimeanza jioni ya siku ya Alkhamisi (11 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (6 Februari 2020m) na zitaendelea kwa muda wa siku tatu, chini ya uhadhiri wa Shekh Abdullahi Dujaili na mwimbaji mashuhuru Haji Qassim Karbalai, na kuhudhuriwa na kundi kubwa la waombolezaji na mazuwaru watukufu.
Katika siku ya kwanza majlisi imefunguliwa kwa Quráni baada ya swala za Magharibi na Isha, kisha Shekh Abdullahi Dujaili akapanda kwenye mimbari na kutoa mawaidha, amezungumza kuhusu utukufu wa Ummul Banina (a.s), na namna alivyo jitolea watoto wake wanne kwa ajili ya kumlinda mjukuu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) siku ya Muharam kumi, kisha wakasimama kuomboleza huku wakipiga vifua na kuimba matam chini ya uongozi wa muimbaji mashuhuri Haji Mula Baasim Karbalai.