Mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa leo (12 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (7 Februari 2020m) iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), chini ya uimamu wa Sayyid Ahmadi Swafi, amesoma nakala kutoka ofisi ya Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu, inayo husu mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa.
Amesema:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.
Enyi mabwana na mabibi.. nakusomeeni nakala iliyotufikia kutoka ofisi ya Mheshimiwa Sayyid katika mji wa Najafu:
Yapasa kuzungumzia mambo mawili yanayo husiana na matukio ya wiki hii:
Kwanza: Pamoja na Marjaa Dini mkuu kutoa mwito mara nyingu kuhusu kuacha kutumia nguvu na kufanya maandamano ya amani, pamoja na kuhakikisha harakati za wananchi wanaodai islahi zinajiepusha kufanya mambo yanayo dhuru watu na kuvunja umoja wa wananchi na kuhurumiana kwao, jambo hilo halijazuwia matukio ya kuumiza kama yaliyo tokea siku chache zilizo pita, damu takatifu imemwagika kinyume na sharia, tukio la mwisho ni lile lililotokea katika mji wa Najafu jioni ya Jumatano iliyopita.
Wakati ambao Marjaa Dini anakemea uvunjifu wa amani wa kila aina, na kuzipa pole familia zilizo poteza wapenzi wao na kuwaombea majeruhi wapone haraka, anasisitiza aliyosema siku za nyuma kua hatuwezi kuacha kutegemea jeshi la serikali katika kuzuwia fujo na vurugu na kujitenga na serikali kwa ujumla, jeshi ndio lenye jukumu la kulinda amani na utulivu, pamoja na kuimarisha amani na utulivu kwenye viwanja vinavyo tumiwa na waandamanaji, waovu wanajipenyeza na kufanya uharibifu jambo hilo halikubaliki, kazi ya kuwazuwia waovu hao ni jukumu la jeshi, wanatakiwa walifanye kwa weledi mkubwa bila kuleta madhara kwa watu wanaofanya maandamano ya amani, pamoja na kuzuwia uharibifu wa mali za umma na binafsi kwa aina yeyote ile.
Pili: Marjaa Dini mkuu katika khutuba iliyo pita alieleza mtazamo wake kuhuna njia nzuri ya kumaliza matatizo ya kisiasa, akafafanua kua serikali mpya itakayo undwa inatakiwa iaminike kwa wananchi na utilize hali na kurudisha haiba ya serikali, na iitishe uchaguzi wa mapema katika mazingira ya amani na utulivu, mbali na kuathiriwa na mitazamo ya nje kwa mali na siraha kinyume na sheria, Marjaa Dini kwa mara nyingine anasisitiza kua haitakiwi kushawishiwa au kupangiwa mambo ya kufanya na watu au mataifa ya nje.