Marjaa Dini mkuu amerudia msimamo wake wa kukemea utumiaji wa nguvu dhidi ya watu wanaofanya maandamano ya amani.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amekemea tena kutumia nguvu dhidi ya watu wanaofanya maandamano ya amani, na amehimiza kufanya maandamano ya amani na kuziepusha harakati za kudai islahi na vitendo vinavyo haribu mali za watu na umoja wa raia na kuhurumiana kwao.

Ameyasema hayo kwenye khutuba ya swala ya Ijumaa leo (12 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (7 Februari 2020m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.

Lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Pamoja na Marjaa Dini mkuu kutoa mwito mara nyingu kuhusu kuacha kutumia nguvu na kufanya maandamano ya amani, pamoja na kuhakikisha harakati za wananchi wanaodai islahi zinajiepusha kufanya mambo yanayo dhuru watu na kuvunja umoja wa wananchi na kuhurumiana kwao, jambo hilo halijazuwia matukio ya kuumiza kama yaliyo tokea siku chache zilizo pita, damu takatifu imemwagika kinyume na sharia, tukio la mwisho ni lile lililotokea katika mji wa Najafu jioni ya Jumatano iliyopita).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: