Marjaa Dini mkuu amesisitiza umuhimu wa serikali mpya ijayo kukubalika kwa raia na itulize hali pamoja na kurudisha haiba ya dola, sambamba na kuitisha uchaguzi wa mapema katika mazingira ya amani na utulivu, wala isiathiriwe na watu au mataifa ya nje kwa mali na siraha, kwa mara nyingine amesisitiza kua haungi mkono mchakato wa kuunda serikali mpya kuingiliwa na watu au mataifa ya nje.
Ameyasema hayo katika khutuba ya swala ya Ijumaa ya leo: (12 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (7 Februari 2020m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hussein (a.s), iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:
(Marjaa Dini mkuu katika khutuba iliyo pita alieleza mtazamo wake kuhuna njia nzuri ya kumaliza matatizo ya kisiasa, akafafanua kua serikali mpya itakayo undwa inatakiwa iaminike kwa wananchi na utilize hali na kurudisha haiba ya serikali, na iitishe uchaguzi wa mapema katika mazingira ya amani na utulivu, mbali na kuathiriwa na mitazamo ya nje kwa mali na siraha kinyume na sheria, Marjaa Dini kwa mara nyingine anasisitiza kua haitakiwi kushawishiwa au kupangiwa mambo ya kufanya na watu au mataifa ya nje).