Maukibu ya watu wa Najafu inaomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s), mbele ya kaburi la mwanae Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mji wa Karbala, kupitia maukibu kubwa ya waombolezaji yenye maelfu ya watu kutoka mji wa kiongozi wa waumini (a.s), nalo ni jambo la kiimani ambalo watu wa Najafu wamezowea kulifanya katika kuomboleza msiba huu mkubwa ndani ya nyoyo za waumini ambao ni wafuasi wa Ahlulbait (a.s).
Watu wa mji wa mbora wa mawasii (a.s) wamemiminika katika kaburi la mnyweshaji wenye kiu -Saaqi Atwaasha- (a.s) wakiwa katika maukibu ya kuomboleza huku wakipiga vifua na kutokwa machozi wakiwa wanaimba kaswida zilizo amsha hisia za huzuni kwa watu wote waliopo ndani ya malalo takatifu, na kusoma riwaya zilizo pokewa kuhusu bibi huyo mtukufu na msimamo wake ulio mfanya kua alama ya huzuni na kujitolea.
Maukibu ikahitimisha maombolezo yake kwa kufanya majlisi ndani ya haram ya Abbasi (a.s) ambayo wameshiriki watu wote waliokuwepo ndani ya haram hiyo.