Miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu
Uwekaji wa dhahabu katika minara ya Atabatu Abbasiyya tukufu
Kutokana na ukongwe wake, na kufuatia kuathiriwa na hewa pamoja na maji, na kutelekezwa kwa muda mrefu kuliko pelekea kuharibika sehemu ya vioo na kuvunjika, sambamba na mipasuko mikubwa iliyokuwepo katika minara ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) jambo ambalo lilikua ni hatari, ikawa ni muhimu kufanya matengenezo ya haraka, mradi wa kukarabati minara hiyo na kuweka dhahabu umekamilika ndani ya miezi 22, nayo ni kazi iliyofanywa kwa namna ya pekee hapa Iraq, uongozi mkuu umebakisha maandishi yaliyo kuwepo katika minara hiyo pamoja na nakshi zake, maandishi hayo yameandikwa upya pamoja na kuwekwa nakshi sambamba na kuzingatia ubora wa kihandisi, eneo lililokua na vioo sasa limewekwa dhahabu iliyotiwa mina, ufunguzi wa minara hiyo ulifanyika katika siku ya kuadhimisha tarehe aliyozaliwa Abulfadhil Abbasi (a.s), ambayo ni tarehe 4 Shabani 1431h.
Zaidi kuhusu mradi
Idadi za habari 7
Zaidi
Picha za mradi
Idadi ya picha 30
Zaidi