Miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu
Mradi wa kuweka marumaru katika kubba tukufu
Kwa sababu ya kuishi miaka mingi jengo la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kutokana na mazingira ya unyevu nyevu na mabadiliko ya hali ya hewa, sambamba na kazi za ujenzi zinazo endelea, yote hayo ni sababu ya kupatikana kwa mipasuko katika kubba hilo, ukizingatia kua jengo ni kubwa na limepanda sana pia halina marekebisho ya mara kwa mara, ndipo uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu ukatoa maelekezo kwa kitengo cha usimamizi wa kihandisi na kitengo cha miradi ya kihandisi ya kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika majengo ya malalo takatifu, ikaundwa kamati maalum inayo fuatilia na kutoa mapendekezo kuhusu swala hilo, baada ya kumaliza matengenezo ya minara miwili mitukufu (kazi iliyo fanywa na shirika la ujenzi la ardhi takatifu), kazi ya kufanya upembuzi yakinifu katika kubba tukufu ikaanza, na ikakabidhiwa ripoti kamili kuhusu ukarabati wa kubba unaohitajika kwa uongozi wa wakfu shia, pamoja na gharama itakayo tumika.
Zaidi kuhusu mradi
Idadi za habari 1
Zaidi
Picha za mradi
Idadi ya picha 12
Zaidi