Miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu
Mradi wa mnara wa saa
Saa iliyopo juu ya mnara wa kwenye paa la mlano wa Kibla ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ambayo ni miongoni mwa saa za turathi za kale, historia yake inaendana na historia ya Atabatu Abbasiyya tukufu, katika zama za Othmaniyya ilipo shambuliwa na saa pia ilishambuliwa na watu hao maadui wa turathi za Ahlulbait (a.s), hadi ikaacha kufanya kazi, ikaharibika tena wakati wa maandamano ya Shaábaniyya mwaka (1991m sawa na 1411h) baada ya vibaraka wa utawala wa kidikteta kushambulia mji wa Karbala kwa siraha nzito na nyepesi, ambapo kubba ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ilishambuliwa kwa siraha nzito na mnara wa saa ukashambuliwa pia, jambo lililo pelekea kuharibika kwa saa hiyo, imefanyiwa matengenezo makubwa lakini haikuweza kurudi kama ilivyokua zamani, baada ya kushuhudiwa kwa miradi ya ukarabati na upanuzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ukiwemo mradi wa upanuzi wa mlango wa Kibla na paa linalo beba mnara wa saa ndipo ikawa muhimu kutekeleza mradi wa mnara wa saa, kazi yake ya awali ilikua ni kuondoa mabaki ya mnara wa zamani bila kuathiri sehemu zingine, na kujenga mnara mpya uliowekwa kwenye kitako cha vyuma (nondo) zilizo sukwa juu ya eneo la mlango, kwa kufuata umbo lake lilelile la pembe nne, juu ya mnara huo kuna kubba ndogo iliyo jengwa kwenye kitako cha nondo zilizo sukwa kwa umbo la pembe nne pia.
Zaidi kuhusu mradi
Idadi za habari 4
Zaidi