Ukarabati na uwekaji marumaru kwenye ukuta wa nje ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)
Miongoni mwa kazi za ukarabati unao endelea katika Atabatu Abbasiyya tukufu zinazo pendezesha muonekano wa eneo hili tukufu, ni uimarishaji wa ukuta wa nje ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi ambayo ni miongoni mwa mradi wa upauwaji wa uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Picha baada ya kukamilika kwa ukarabati na uwekaji wa marumaru: Ukuta wa nje wa haram ya Abulfadhil
Atabatu Abbasiyya tukufu imeshuhudia miradi mingi, miongoni mwa miradi hiyo ni kukarabati kwa jengo la malalo matukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wahandisi mahiri wametekeleza makumi ya miradi ya ukarabati, miongoni mwa ...