Miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu
Mradi wa upanuzi wa jengo la Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kuongezwa kwa eneo jipya katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuingiza idadi kubwa zaidi ya mazuwaru wanaokuja kufanya ibada ya ziara, swala na dua, pia kuifanya iendane na maendeleo na upanuzi wa shughuli za vitengo na idara za Ataba baada ya 9/4/2003m, katika sekta za uhandisi, elimu, utumishi, uratibu, mali na zinginezo, na kuongeza majengo ya chini ya Ataba tukufu, baada ya kufikiwa makubaliano na kutengwa pesa za kutekeleza mradi na uongozi wa wakfu Shia, idara ya Atabatu Abbasiyya ikaanza kutekeleza mradi, wakati wa utekelezaji wa mradi mazuwaru wametengewa sehemu ambazo wanaendelea na ibada bila tatizo huku ofisi za vitengo zikiendelea kama kawaida, baada ya kumaliza upanuzi huo zitahamia katika eneo la upabuzi na sehemu zilipo sasa hivi itatumiwa na mazuwaru kufanya ibada. Kwa mujibu wa vipimo vya kihandisi eneo la ardhi inayo ongezwa karika Atabatu Abbasiyya ni zaidi ya mita za mraba (10,000) zinajengwa kwa urefu jengo la ghorofa tatu, jumla ya ukubwa wa eneo lililo ongezwa litakua mita za mraba (30,000) sawa na asilimia 25% ya eneo la Atabatu Abbasiyya tukufu, limewekwa vitu vyote muhimu vya kisasa, kuanzia kwenye sardabu (jengo la chini), ghorofa la kwanza, la pili na la tatu, upanuzi huo unafaida nyingine ambayo ni kumalizika kwa tatizo la kutiririka kwa maji, lililokua likiisumbua Atabatu Abbasiyya, imewekwa mifumo ya njia za maji kwenye sardabu chini ya ardhi, na kuna pampu za kusukuma maji na kuyapeleka katika visima kwa kutumia mitambo maalum.
Zaidi kuhusu mradi
Idadi za habari 52
09-01-2017
Zaidi
Picha za mradi
Idadi ya picha 584
Zaidi
Video za mradi
Vipande vya video 1