Miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu
Sardabu ya Imamu Aljawaad (a.s)
Katika yaliyo pangwa kwa umakini mkubwa kwenye Ataba za Karbala tukufu, ni kuanzisha mradi mgumu zaidi katika Ataba za Iraq, wahandisi wa Iraq kwa mara nyingine wanakamilisha kazi zilizo anza kufanywa na babu zao za ujenzi wa Ataba na mazaru, mara hii wanajenga uwanja wa haram chini ya ardhi katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa jina la: (Sardabu ya Imamu Aljawaad –a.s-). Mradi mgumu chini ya ubunifu mpya na ujengaji wa wakisasa, ni ujenzi unao fanyika kwa mujibu wa mazingira na mahala, Ataba za Karbala hupokea mazuwaru wengi na hakuna wakati ambao watu huisha ndani ya Ataba hizo, kwa hiyo kufanya ujenzi wa aina hiyo ni jambo gumu na kuukamilisha ni mafanikio makubwa, kwani kuna ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu kila mwaka pia kuna ziara zinakaribia kua za mamilioni ya watu kila wiki ukiongeza na maelfu ya watu kila siku katika eneo lisilozidi (2m6400), pamoja na upanuzi unaoendelea, sasa umehamia chini ya ardhi, ili kuwezesha kuingia idadi kubwa zaidi ya mazuwaru.
Zaidi kuhusu mradi
Idadi za habari 3
Zaidi
Picha za mradi
Idadi ya picha 21
Zaidi